About Us

Tanzanite Society

Jumuiya ya Watanzania - Japani

 

 

UTANGULIZI

“Umoja ni nguvu.” Ni msemo wa Kiswahili unaotoa wito wa kuunganisha nguvu ili

kuwa na mshikamano zaidi na hatimaye kufanikisha malengo ya maisha na kujiletea

maendeleo kwa ujumla. Ni kinyume cha msemo, “utengano ni udhaifu.” Watanzania

wanaoishi nchini Japani wanahitaji umoja zaidi ili waweze kusaidiana kikamilifu katika

masuala mbalimbali. Vilevile wanahitaji kubuni mbinu na mikakati inayoweza kuleta

maendeleo yao wanapokuwa nchini Japani na pia kusaidia kubuni mikakati ya kuleta

maendeleo ya kitaifa nyumbani Tanzania.

 

MADHUMUNI

Madhumuni na malengo makuu ya Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Japani

yatakuwa yafuatayo:

(a) Kujenga mshikamano baina ya Watanzania wanaoishi Japani.

(b) Kusaidiana katika shida na raha.

(c) Kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali kama vile utalii, utamaduni

na kadhalika.

(d) Kuwaunganisha Watanzania na Wajapani pamoja na raia wa nchi nyingine

wanaoishi Japani.

(e) Kushauriana na kubuni shughuli mbalimbali zenye malengo ya kuleta

maendeleo nyumbani Tanzania.

(f) Kutangaza Jumuiya kwa Watanzania wanaoishi sehemu mbalimbali za

Japani na wale wanaotegemea au wanaokuja kuishi nchini Japani.

(g) Kujenga jina zuri la Tanzania nchini Japani.

 

KUJIUNGA

Ili kujiunga na Jumuiya hii ni lazima

(a) Uwe Mtanzania.

(b) Uwe umepata uwanachama wa heshima.

(c) Uwe unaishi nchini Japani.

(d) Uwe umelipa kiingilio.

(e) Uwe umekubaliana na Katiba ya Jumuiya.

Tanzanite Society

 

1. Wajue Viongozi wake

 

2. Dira na Malengo ya Jumuiya

 

3. Mlezi wa Jumuiya - Ubalozi wa Tanzania Japani

 

4. Kujiunga na Jumuiya

 

5. Jiunge nasi kupitia Facebook

 

6. Moderator

7. Blog and Photo gallary

 

8. Andikisha taarifa zako hapa

Habari na Matukio

1. Mkutano wa viongozi wa jumuiya ubalozini tarehe 11 Mei 2014 kuanzia saa nane mchana. Tuhudhurie wote bila kukosa.

 

2. Mkutano wa Watanzania WOTE siku ya Jumapili tarehe 18/05/2014 kuanzia saa nane kamili (8:00) mchana katika ukumbi wa ubalozi wetu kule Setagaya. Mkutano huu ni muhimu sana kwani utajadili masuala yanayohusiana na maendeleo ya Jumuiya yetu ikiwa ni pamoja na nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zimeachwa wazi kwa sababu mbalimbali na maandalizi ya mapekezi ya ugeni wa Makamu wa Rais ikiwa ni pamoja na kukubaliana juu ya ujumbe tutakaotaka kumpatia atakapokutana nasi.

 

Mkutano

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Mohammed Gharib Bilal atakutana na Watanzania wote waishio Japani - Tarehe 21/5/2014. Soma juu kwa maelezo zaidi

Get to Know Tanzania

 

 

1. Jina : Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Name: United Republic of Tanzania

2. Mahala: Afrika ya Mashariki

Location: Eastern Africa

 

3. Lugha Maalum: Kiswahili, Kingereza

Main Languages: Swahili, English

 

4. Idadi ya Watu : Milioni 46 ( Makadirio)

Population: Approx. 46Million

 

5. Sehemu za kutembelea Tanzania

Place to visit in Tanzania

 

Zaidi/More...

COPYRIGHT © 2014 | ALL RIGHTS RESERVED

PRIVACY STATEMENT | TERMS & CONDITIONS